Featured

    Featured Posts

FAHAMU ZAIDI CHIDI BENZ KUKAMATWA AIRPORT NA DAWA ZA KULEVYA.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika leo.
Chidi amekamatwa jana mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo ambapo alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae pia kijiko na Chid Benz amekiri mwenyewe kuwa hizo dawa ni zake pamoja na hivyo vifaa
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana