Featured

    Featured Posts

DIAMOND PLATNUMZ KUTUNUKIWA PHD KUTOKA IDARA YA SANAA YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

10320592_734058296615987_8100202072456761249_n
Tarifa kutoka Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zinasema kuwa tarehe 8 Novemba 2014, Kijana Nassib Abdul atatunukiwa Shahada ya Uzamivu(Phd) na Chuo hicho kwa kuthamini mchango wake kwenye jamii kupitia sanaa.(Honorary PhD in Fine &Perfoming Arts).
Alongside DIAMOND mwingine atakayepewa Shahada hii ya Heshima kwenye Mahafali haya ni Balozi Fulgence Kazaura (marehemu) ambaye aliwahi kuwa Chancellor wa UDSM miaka ya nyuma!!
Naibu Mkuu wa shule ya Sanaa na Sayansi ya Jamii (College of Arts and Social Sciences) Prof.H Sigala amekiri kupokea maombi kutoka Idara ya Sanaa za Maonesho (Department of Fine &Perfoming Arts) ya kumtunuku Diamond PhD.
Amesema bado haijadhibitika kama Diamond atatunukiwa shahada hiyo hadi bodi ya taaluma ya chuo (senate) ikae na kupitia maombi hayo. “Senate ikikaa inaweza kukubali au kukataa maombi hayo, lakini kwa sasa hatuwezi kusema lolote” alisema Prof.Sigala.
Mashabiki wa Diamond wamepokea kwa furaha taarifa hizi na wengine wameanza kurusha vijembe mitandaoni kujibu mapigo ya waliomzomea Diamond kwny tamasha la Fiesta mwaka huu.
Mdau mmoja wa karibu wa Diamond amenukuliwa kwny ukurasa wake wa Facebook akisema “Ningependa kuwakaribisha Wazomeaji woooteee wenye sauti mbaya sana waweze kufika kwenye Viwanja vya UDSM kushuhudia Tukio la Kihistoria kwa Mtoto huyu wa Tandale ambaye ni BIDII NA HESHIMA Vimemfikisha hapa.”
Ikiwa “Senate” ya UDSM itapitisha maombi hayo, na Diamond kutunukiwa Shahada hiyo basi atatambulika rasmi kama DR.NASIBU ABDUL au Pengine DR.DIAMOND PLATNUMZ au ukitaka swaga unaweza sema DR.PLATNUMZ BABY!
Baadhi ya watu wameonekana kutoridhishwa na mapendekezo hayo ya Idara ya Sanaa ya chuo kikuu cha Dar kumtunuku Diamond PhD, huku wengine wakinukuliwa wakisema “Ukistaajabu Uprofesa wa JK utaona PhD ya Diamond”
source:Jf
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana