Featured

    Featured Posts

Shilole Atoboa Sababu ya Kuuza Nyumba Yake Aliyokua Anajenga Kimara


Shilole Atoboa  Sababu ya Kuuza Nyumba Yake Aliyokua Anajenga Kimara
Msanii Shilole aliwai kuingia kwenye headlines baada ya ku-post kwenye instagram picha ya nyumba yake ambayo alikua bado anaijenga. Caption ya picha hiyo ilikua inasomeka hivi, “Mungu nisaidie nimalize hii kitu ili watoto wangu wasije kupata tabu”.
Eneo ambalo alilokua anajenga nyumba hiyo ni Kimara jijini Dar es Salaam lakini Shilole amesema kwamba ameuza nyumba hiyo ambayo ilikua bado haijaisha vizuri.

Akiongea na millardayo.com Shilole ametoa sababu za kuuza nyumba hiyo kama hivi, “Nyumba yangu niliyokua naijenga maeneo ya Kimara nimeiuza kwenye hatua iliyofikia kama ilivyokua inaonekana kwenye picha. Sababu ya msingi iliyonifanya kuiuza ni kwamba pale eneo nililokua najenga ni nimegundua kwamba ni njia ya maji. Hivyo basi sitaki kupata tabu msimu wa mvua ukianza maji yakiwa yanapita nje ya nyumba yangu. Pia hakuna tatizo nimeuza nitajenga kwingine mambo ni mazuri”
Shilole Atoboa  Sababu ya Kuuza Nyumba Yake Aliyokua Anajenga Kimara 1
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana