Featured

    Featured Posts

Wafuasi wa UKAWA Wavamia Msafara wa Magufuli Jijini Arusha Huku Wakiimba Lowassa!!!.....Lowassa!!........Mabomu Yarindima, 6 Watiwa Mbaroni

Mgombea  Urais  wa  Chama  cha  Mapinduzi  (CCM)  yuko  jijini  Arusha  ambapo  jioni  hii yupo  katikati  ya  jijini hilo  ndani  ya  uwanja  wa  Sheikh Amir Abeid,  akinadi  sera  za  chama  chake.


Kabla ya kufanya mkutano kwenye uwanja wa Sheikh Amir Abeid  jioni  hii, Dk. Magufuli alielekea kwanza wilayani Monduli leo asubuhi ambako alitakiwa  kufanya  mkutano wa hadhara katika eneo la Mto wa Mbu  kwa  mujibu  wa  ratiba  yake.

Taarifa  tulizozipata  zinaarifu  kuwa  hali  haikuwa  nzuri  katika  eneo  hilo  la  Mto  wa  Mbu  baada  ya  msafara  wake  kukumbana  na wafuasi  wa  UKAWA  ambao  walivamia  msafara  huo  na  kuanza  kushangilia  wakisema  Lowassa!!!....Lowassa!!  Lowassa!!!  huku  wakiwa  wamenyoosha  vidole  viwili  juu.-Tazama  Video  Hii


Hali  hiyo  iliwafanya  polisi  waingile  kati  kwa  kupiga  mabomu  ya  machozi  ambapo  vijana  kadhaa wametiwa  mbaroni  wakituhumiwa  kuhujumu  mkutano  huo  wa  Magufuli.- Tazama  na Hii 

Mbali  na  matukio  hayo, Magufuli  amefanikiwa  kuliteka  jiji  la  Arusha  na  Watu  wamefurika  vya  kutosha  ndani  ya  uwanja  wa Sheikh Amir Abeid
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana