Featured

    Featured Posts

ROSE NDAUKA KANUMBA FEKI, WAZUA GUMZO!KUMBE NI WAPENZI

GUMZO! Waigizaji vinara ndani ya Bongo Movies, Rose Ndauka na Rammy Gallis ‘Kanumba Feki’ wameibua gumzo na minong’ono kufuatia kugandana na mara nyingi kuonekana peke yao huku mazungumzo na mapozi yao yakikoleza hisia kwamba, huenda ni wapenzi, Amani lilikuwepo.

 Waigizaji vinara ndani ya Bongo Movies, Rose Ndauka na Rammy Gallis ‘Kanumba Feki’ wakikata keki.
Gumzo hilo liliibuka Oktoba 7, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Jozi Village, Msasani, Dar kulikokuwa na sherehe ya kuzaliwa kwa wawili hao ambapo watu mbalimbali, wakiwemo mastaa wenzao wa filamu walikuwepo na kuonekana kushangazwa na ukaribu uliopitiliza wa wasanii hao.
Aidha, Rose na Kanumba Feki (Gallis) walithibitisha kuwa na ukaribu usiofaa baada ya kila mara kuwakimbia waandishi wetu wanapowakaribia jambo lililoongeza mshangao mkubwa.
Awali, wasanii hao hawakuonesha dalili yoyote zaidi ya kuzungumza kawaida na kujichanganya na mastaa wenzao, lakini kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kuyoyoma, ndipo ukaribu na mapozi ya kutia shaka yalianza kuonekana!
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya wageni waalikwa walisikika wakiguna na kuzungumza namna ambavyo ukaribu na mapozi ya Rose na ‘Kanumba’ yanavyoacha viulizo vingi kuliko majibu na wengine wakienda mbele zaidi kwa kutamka kuwa, wasanii hao wamekuwa wakitoka kimapenzi kwa muda mrefu sasa.
“Mh! Jamani mbona mapozi yao yanachanganya sana, maana kadiri muda unavyosonga mbele nawaona wakigandana zaidi na kupelekana chobingo, tena wanasogeleana kwa ukaribu wa kimapenzi,” alisikika msichana mmoja akizungumza na wenzake waliokuwa karibu na waandishi wetu.
“Mbona ni wapenzi wa muda mrefu hawa, sisi tunajua tangu zamani na wala hatuoni ajabu kuwaona katika ukaribu na mapozi hayo ya kimahaba,” alisema msanii mmoja wa kike mwenye jina kubwa Bongo.
Wiki imekatika, Amani lilikuwa likiwasaka wote ili kujua tofauti ya tui na maziwa juu ya uvumi na mapozi hayo tata ambapo siku ya tukio hawakuwa tayari kuongea. ‘Vidudumizi’ wetu walimbana Rose kwa maswali magumu ambapo alikanusha kuwa na uhusiano usiofaa na Kanumba na kushikilia alichokiita, ‘marafiki wa muda mrefu’.
“Jamani, sisi ni marafiki tu na si unajua hii ni sherehe yetu wote, yaani tarehe zetu za kuzaliwa zinafanana na ndiyo maana tumeamua kuifanya pamoja. Hakuna zaidi ya hapo. Sisi ni marafiki wa muda mrefu,” alisema Rose.
“Aah! Babu ee achana na mimi bwana, hata kama sisi ni wapenzi, inakuhusu nini bwana? Chukua time,” alilalama Kanumba Feki.
Gallis alianza kuwika katika ulimwengu wa filamu mara baada ya kifo cha nyota wa tasnia hiyo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Aprili 7, mwaka 2012 akifananishwa kwa sura (eti) na marehemu huyo. Ameshatoa filamu kadhaa, lakini iliyo sokoni kwa sasa na ‘kukimbiza’ inaitwa Zakayo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana