Featured

    Featured Posts

Kaka wa Jenerali MWAMUNYANGE Naye Afunguka Kuhusu Mdogo Wake Kulishwa Sumu

KAMISHINA Msadizi na Mwandamizi mstaafu wa Jeshi la Polisi, Aden Mwamunyange ambaye ni kaka wa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange, naye amekanusha taarifa zilizoenezwa hivi karibuni katika mitandao ya jamii kuwa amelishwa simu.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Jeti Lumo, Dar es Salaam juzi, alisema hizo taarifa hizo si za kweli na ni uzushi.
“Mimi kama mwana familia nakanusha taarifa hizo zinazosambaa mitandaoni, habari hizo hazina ukweli hata kidogo.

“Jenerali Mwamunyange ni mzima wa afya, anaendelea na shughuli zake kama kawaida na yuko nje ya nchi kwa safari za kazi,” alisema Aden.
Alisema ni kawaida kwa Jenerali Mwamunyange kumuaga kila anaposafiri na kama kaka yake alimuaga kuwa alikuwa anasafiri kikazi kwenda nje akianzia Italia.

Pia alikanusha taarifa zilizosema kuwa ukoo wao umepewa fedha kuzima taarifa za Jenerali Mwamunyange na akawataka wananchi kuzipuuza.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana