Polisi wakiwa wamesimamisha msafara wa Lowassa
Polisi wakiwa tayari kwa lolote baada ya kuzuia msafara wa
Msafara ukiwa umesimama
Viongozi wa upinzani waliokua katika msafara huo pichani Mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema
Mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema akisalimiana na Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI James Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akijaribu kuzungumza na Polisi.
Mwenyeiti wa NCCR-MAGEUZI Mbatia akifafanua jambo kwa Wanahabari kuhusiana na zuio hilo la Polisi.
Edward Lowassa akizungumza na wanacham wa vyama mbalimbali waliojitokeza kumlaki na kumsimamisha katika eneo la Boma Ng'ombe.
Lowassa akizungumza kwa simu huku akiwa na Mbunge wa Moshi Mjini Mzee Philemon Ndesamburo.
********
Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa ameshindwa kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe hayati mzee Peter Kisumo yaliyokuwa yanafanyika Usangi mkoani Kilimanjaro baada ya msafara wake kuzuiliwa na polisi katika wilaya ya Mwanga kutokana na kuongozana na wananchi wakiwemo vijana waliokuwa na pikipiki waliokuwa wanakwenda kwenye mazishi.Gari la Mh Lowassa ambaye pia ni mgombea urais wa Chadema akiwakilisha Ukawa lilianza kufuatwa na magari mengine ya watu binafsi na pikipiki baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akitokea na Dar es Salaam na alipofika Moshi kundi la vijana walifunga barabara na kulazimika kuingia katika hotel ya kizi ambako pia walimfuata na kuzingira lango kuu na licha ya kuwasihi kuwa wampe nafasi aende kwenye mazishi vijana hao waliendelea kulifuata gara lake.
Katika hali ambayo sio rahisi kuamini vijana hao wakiwa na pikipiki waliendelea kufuata gari la Mh Lowassa hadi Mwanga na alipoanza safari ya kuelekea Usangi takrbani kilometa moja kutoka barabara kuu polisi wakafunga barabara hali iliyosababisha mvutano mkubwa na jambo ambalo limelalamikiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya viongozi akiwemo mwenyekiti wa NCCR mageuzi James Mbatia na Mh Agustino Mrema.
Baada ya vuta nikuvute kati ya polisi na wananchi na viongozi hao wa vyama vya siasa mkuu wa polisi wa wilaya ya Mwanga aliruhusu watu waliokuwa na pikipiki kuendelea na safari kwa masharti ya kuondoa bendera za vyama vyao na pia kwenda bila msafara maelekezo ambayo licha ya kubalika utekelezaji wake ulikuwa mgumu na kusababisha kuendelea kwa malumbano na ndipo Mh Mbatia akata taarifa za Mh Lowassa kusitisha safari na kuamua kurudi Moshi na hatimaye Dar es Salaam.
Post a Comment