Malori ya kutosha yameshafikisha mamilioni ya bia maarufu kama Budweiser, Miller Lite, Corona na Tecate kwenye hotel ya MGM Grand ambapo pambabo la Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao usiku wa May 2 huko LasVegas.
Hizo brand tofauti za bia zimelipa zaidi ya $5milioni ili kuwa moja kati ya wadhamini wa pambano hilo. Baadhi ya watu waliowai vyumba vya kawaida wamepata kwa bei ya $1600 kwa usiku wa Ijumaa na Jumamosi.
Uongozi wa hotel umesema kwa historia ya mapambano yaliyopita na ukifananisha na hili wanategemea watu zaidi ya 50,000 kufika usiku huo. Pia kuna wafanyakazi wapya 14,000 wameongezeka maalum kwa ajili ya usiku huu.
Pambano hili litahusisha wasanii wengi sana wa hiphop ambao wataenda ku-support Mayweather na wageni wengi wa hali ya juu. Rais wa hotel hiyo anasema kwamba usalama wa wageni ni wa hali ya juu.
Post a Comment