Muimbaji wa Jahazi, Leila akiimba Wimbo wa Fanya Yako.
KUNDI linalotikisa kunako miondoko ya Pwani, Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf leo limefunika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live katika shoo maalum ya Usiku wa Wapendanao 'Valentine's Day'.
Jahazi walianza kutawala jukwaa ambapo, Leila alikuwa wa kwanza kupanda na kuimba Wimbo wa Fanya Yako kisha akafuatiwa na Mwansiti na Fatuma Nyoro. Baadaye alipanda Mzee Yusuf kwa Wimbo wa My Valentine na kufanya ukumbi wote kulipuka kwa shangwe. Mzee Yusuf aliamsha shangwe zaidi baada ya kuimba Wimbo mpya wa Mahaba Niue.
Post a Comment