Mrembo na muigizaji wa filamu, Faiza Ally ambae ni mama wa mtoto mmoja amezibandika picha hizi kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa maeneo ya ufukweni mjini Bagamoyo.
Mbali na ukweli kuwa hapa amevalia nguo za ufukweni, mahabiki wengi wamemshabulia kuwa mavazi haya hayafai kwani yeye sasa hivi ni mama tena amezaa na Muheshimiwa, huku wengine wakisema hapo ndio mahali pake na wa muacha afurahie maisha yake.
Japokuwa ni kweli kuwa Faiza aliwashangaza wengi mwaka jana kwa kuvalia “pampers” kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, lakini kwa hizi nadhani tumwache, amependeza sana. Sijui wewe umezionaje!!.
Post a Comment