Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini
hii na baadae watu wangu francis_ayo na abdul8819 wa pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA !! thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa.
Post a Comment