Featured

    Featured Posts

MAJANGA:DIAMOND ATUPIWA JINI BADALA YAKE LAMPATA MAMA YAKE MZAZI

Imevuja! Kuna madai kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametupiwa jini lakini likamkosa na kumpata mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ kisha kumsababishia ‘gonjwa’ la ajabu, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, watu wanaodaiwa kuwa ni wabaya wa Diamond (Anti-Diamond) walimtupia jini staa huyo lakini bahati nzuri likamkosa na kwa bahati mbaya likampata mama yake ambaye alipata ugonjwa wa kupooza ghafla.
“Ujue kumekuwa na sintofahamu kwa muda mrefu juu ya ugonjwa wa mama Diamond lakini habari za uhakika ni kwamba, mama Diamond yupo hoi baada ya kutupiwa jini ambalo mlengwa wake alikuwa Diamond.
“Mungu tu hakupenda limpate Diamond lakini inasemekana kwamba jini hilo ni hatari endapo lingempata Diamond kwa jinsi lilivyokuwa, basi pengine leo tungekuwa tunazungumza mengine,” kilisema chanzo hicho.
DIAMOND ALIJUA ‘MCHEZO’ HUO?
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, Diamond alijua kwamba mama yake ametupiwa jini ndiyo maana alikuwa akisuasua kutoa uamuzi wa kumuwahisha nchini India kwa matibabu ya hospitali.
“Diamond alijua kuhusu mpango huo wa wabaya wake kutaka kummaliza kishirikina ndiyo maana hakutaka kumkimbiza haraka hospitali na badala yake alijikita kwenye swala na dua kwani yeye anaamini katika dini zaidi,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, baada ya kutafakari kwa umakini wa hali ya juu, imeelezwa kwamba, Diamond alilazimika kumpeleka mama yake nchini India na kupatiwa matibabu kisha kurejea nchini.
ALIRUDI MZIMA
Kwa mujibu wa ndugu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, hivi karibuni (kabla ya Valentine’s Day), mama Diamond alirejea nchini akiwa na afya njema lakini siku chache baadaye alizidiwa tena na kurudishwa India huku ndugu wakijawa na hofu.
“Alirudi Bongo lakini hakukaa sana akazidiwa tena tukalazimika kumrudisha India kwani hali ilizidi kuwa mbaya. Tumekuwa hatutaki kueleza sana juu ya suala hili maana Diamond mwenyewe hapendi haya mambo yajulikane,” alisema ndugu huyo.
DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya chanzo hicho kuvujisha ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimvutia waya Diamond ambapo alikiri kwamba mama yake yupo India lakini hakutaka kulizungumzia zaidi eneo hilo badala yake akaanza kushusha lawama kwa wale aliodai wanamsema vibaya.
“Mama bado yuko kwenye matibabu nchini India na hali yake kusema kweli si nzuri, naomba hapo nisizungumzie sana. Kuhusu masuala ya kutupiwa jini, mimi namuamini Mungu, naamini mama atapona.
“Inaniuma kila siku ninaposikia watu wanaongea vitu ambavyo si kweli na kwa namna nyingine nashindwa kujibu vitu ambavyo mwenyewe sivijui hivyo yote namwachia Mungu, maana yeye ndiye jibu la yote.
“Halafu pia kuna muda ufike, watu wawe wanafahamu mimi pia ni binadamu kama binadamu wengine, wasiwe wananijazia vitu utafikiri mimi sina moyo, wawe waelewa, sipo katika kipindi kizuri kwa sasa na si kila kitu wanachosikia au kuona lazima mimi nikizungumzie, kuna mambo mengine ni ya ndani ya ukoo na yako juu yangu sana, hivyo ukiona kimya simaanishi kuna watu nimewadharau,” alisema Diamond.
TUMEFIKAJE HAPO?
Hivi karibuni kuliibuka madai kwamba kwa makusudi Diamond alishindwa kuhudhuria msiba wa baba Abdul Sykes ‘Dully’ na badala yake picha zikavuja zikimuonesha akiwa kisiwani Zanzibar na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari’ kitu ambacho mwenyewe alikikanusha.
“Si kila picha unayoiona katika mtandao wa kijamii basi itakuwa imepigwa muda huo, inaweza kuwekwa leo kumbe ni ya muda mrefu,” alisema Diamond.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana