Featured

    Featured Posts

MAJANGA HAYA .. DUME LAVAA KIMINI NA SIDIRIA.. LAKATA VIUNO JUKWAANI WANAWAKE WAPIGWA NA BUTWAA


Dume zima ovyoo ! Katika hali ya kushangaza,
mwanaume mmoja ambaye jina lake
halikupatikana mara moja amezua kizaazaa
ukumbini baada ya kutinga akiwa amevalia
nguo za kike na kuonekana kama mwanamke.
Mwanaume huyo tata ( kulia ) akikata mauno.
Mwanaume huyo aliyepachikwa jina la Jike
Dume hilo alinaswa na Amani katika Ukumbi
wa Flamingo ulipo Magomeni, Dar , wiki
iliyopita wakati Bendi ya Extra Bongo ‘ Wazee
wa Kizigo Staili’ ilipokuwa ikitoa burudani
ambapo jamaa huyo alikuwa amevaa sketi na
blauzi ya kike huku kichwani akiwa ametupia
wigi.
Katika hali ya kushangaza, mwanaume huyo
alionesha hana chembe ya aibu kwani alikuwa
akikata mauno mbele ya jukwaa na wakati
mwingine aliwakatia viuno wanaume
wenzake. “ Duh! Kweli dunia imefika ukingoni
jamani , hebu mwangalie yule mwanaume
amevaa nguo za kike utadhani mwanamke
halafu anawakatikia mauno wanaume wenzake
bila hata aibu , ” alisikika mmoja wa waudhuriaji
wa shoo hiyo .
Baada ya kukwepa kunaswa na kamera yetu
mara kadhaa baadaye ilifanikiwa kumnasa
akikata mauno kwenye steji huku akirembua
macho yaliyochorwa wanja na mdomo
uliopakwa lipstiki kama mwanamke .

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana