Mwigizaji wa vichekesho wa kundi la Orijino Komedi,Lucas Mhavile, ‘Joti’, amedaiwa kumvisha pete mpenzi wake wa siku nyingi, ikiwa ni ishara na dalili njema kuelekea kwenye kufunga ndoa.
Picha iliyosambaa mtandaoni inaonyesha akiwa na swahiba wake wa siku nyingi, Mr. Mjuni Sylvatory a.k.a Mpoki, Joti ameonekana mwenye furaha muda wote kwa kutimiza tendo hilo huku akiwa amealika watu wachache sana kuhudhuria tukio hilo.
Hata hivyo Clouds FM imemtafuta Joti kuzungumzia picha hiyo kwenye simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.
Post a Comment