STAA mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula Johari amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi Ray bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu. Akizungumza na Uwazi, Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui mwanaume gani wa kumuoa bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama mwanamke.
Kwanza sihitaji mwanaume wa kunioa awe staa hata siku moja, nataka tu awe wa kunijali na kunithamini na kingine awe mchapakazi kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtafutaji, alisema Johari.
Awali, Johari aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nyota wa filamu, Ray na kuachana baadaye. Kama ni hivyo basi mapenzi yao yalikuwa ni ya boyfriend na girlfriend na wala si ndoa.
Post a Comment