Skendo haziko mbali na kivuli cha staa, hii iko duniani kote na safari hii imemkuta jamaa ambaye wengi wanaofanya Hip Hop wanamuangalia kama model wao, kutokana na nguvu yake kubwa kwenye muziki huo, leo zimeanza kusikika za upande wa pili ambazo huenda hattukuwahi kuzisikia siku za nyuma.
Shawn Corey Carter ama Jay Z tunajua kuwa ana ndoa na mpenzi wake ambaye ni Beyonce na wana mtoto mmoja, ya mitandaoni leo ni ishu ya jamaa mmoja ambaye ana umri wa miaka 21, Rymir Satterthwait ambaye amelalamika kwamba Jay ni baba yake mzazi na amemtelekeza.
Story za mtoto huyo zilianza kuchukua headlines December mwaka jana huku ikihusishwa na ishu ya ugomvi wa Jay Z na Solange kwenye lift, wanadai ishu ya mtoto huyo ilifika mpaka Mahakamani lakini mwanasheria wa Rymir amesema Jay na mwanasheria wake ambaye ni Lise Fisher walipeleka vielelezo vya uongo Mahakamani New Jersey ili kufuta kesi hiyo.
Mama wa mtoto huyo anaitwa Wanda amesema alikuwa na na uhusiano na rapper huyo miaka ya 90.
Post a Comment