Msanii maarufu wa Bongo flavor, Mez B, aliyekuwa mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kurudishwa nyumbani na mama yake, amefariki dunia. Mez B alikuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu na alikuwa kwenye dozi na leo ilikuwa siku ya tatu toka aanze kutumia dawa hizo.
Leo asubuhi aliamka na kunywa dawa na chakula, ila hali yake haikuwa sawa na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa siku na kuamuru awekewe drip, lakini hali yake ikawa mbaya zaidi. Wakati wanampeleka hospitalini, alifia mapokezi.

Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen.
Post a Comment