KAMA kawaida wadau wa safu bora kabisa ya
Sindano Tano, kutokana na maombi yenu leo
tumemleta yule mwanadada kipenzi cha wengi
Aunt Ezekiel amefungukia maswali matano .
Mwanadada kipenzi cha wengi Aunt Ezekiel .
Paparazi: Mambo vipi ? Kwema lakini Aunt?
Ehne leta maneno, mna mipango gani na baba
mtoto mtarajiwa , Iyobo?
Aunt: Hahaha mimi mzima! Kuhusu Iyobo,
mh! Kanipa mimba ! Si kweli , nitakapojifungua
nitamtaja baba wa mtoto wangu.
Paparazi: Mbona Iyobo amekuwa akijinadi
kwenye vyombo vya habari kuwa mzigo
ulionao ni wake ?
Aunt: Mh! Jibu langu ni hilo nililokupa .
Paparazi: Msanii gani wa kike ambaye
unamkubali sana Bongo.
Aunt: Kwa kweli namkubali sana Wema
Sepetu.
Aunt Ezekiel akiwa na Mose Iyobo.
Paparazi: Hivi kabla ya kuingia kwenye ‘ u -
miss ’ ulikuwa unafanya shughuli gani ?
Aunt: Nilikuwa nishaanza uigizaji ndipo
waandaaji wa mashindano ya u-miss
waliponiona na kuniambia nafaa na baada ya
hapo nikashiriki kule Ilemela , Mwanza .
Paparazi: Ukiambiwa utoe ushauri juu ya penzi
la shemeji yako wa zamani Diamond kwa
mpenzi wake wa sasa Zari , utawaambiaje ?
Aunt: Hahaha ! Jamani hapo kwa kweli ‘ no
comment ’ .
Post a Comment