Diamond ambaye wakati msiba huo unatokea alikuwa Zanzibar na mpenzi wake Zari, ameelezea sababu zilizomfanya kushindwa kuhudhuria mazishi.
“Watu waliniona niko zanzibar lakini walikuwa hawajui nimeenda kufanya nini,” Diamond ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM. “Usiangalie kila unachokiona Instagram ukajua mtu labda kwasababu alikuwa anafanya starehe. Niko katika kipindi ambacho sio kizuri kwangu mimi na familia yangu kwasababu kuna vitu ambavyo siwezi kuvizungumza lakini, na siwezi kuviweka kwenye media ndo maana watu wengine wanaweza kuniona nacheka lakini […] kwanza mama yangu anaumwa na anaumwa sana sijawahi kulizungumza hili ndo nalizungumza hapa, hapa ninapoongea na wewe yupo India, kuna vitu vingi vinaendelea, siwezi kusema nilikuwa Zanzibar nafanya nini, inawezekana ikawa ndo sababu iliyonifanya mpaka mimi nikachelewa kwenda kwenye msiba, lakini inawezekana labda mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kutoa pole katika social networks zangu mimi.”
“Unajua wakati mwingine ni vizuri kwenda kuzika lakini inawezekana mtu akawa ameenda kuzika lakini mi nikawa sijaenda kuzika nikawa nimefanya kitu cha maana kuliko wale walioenda kuzika kwasababu huwezi kujua nilifanya kitu gani. Nilisikia niliambiwa watu walikuwa wanongea sijui Diamond hajafika lakini naamini kuna watu wengi hawakufika na kila mtu hakufika kwa sababu fulani. Dully mi ni kama kaka yangu kabisa ni mtu ambaye amenisaidia vitu vingi sana isingewezekana kabisa niko ninanafasi nishindwe kwenda kwenye msiba.”
“Ukiacha tu Dully mwenyewe kwanza mtu aliyefariki ni kama mzee wangu, na mtu ambaye amefanya kitu kikubwa katika sanaa hii ya muziki na mimi nimefika hapa yeye pia ana mchango wake, so haikuwa rahisi eti mimi nisiende tu nikiwa sina sababu, kulikuwa na sababu na ndio maana.” Alimaliza Diamond.
Post a Comment