Featured

    Featured Posts

BEI YA PETROLI DAR YASHUKA HADI......


Hii ni mara ya pili katika kipindi cha siku 28 kwa Ewura kushusha bei, mara ya mwisho ilikuwa Januari 7, iliposhusha kutoka Sh2,097 hadi Sh1,955 kutokana na kushuka kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia.

Akitangaza bei mpya, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema bei ya petroli imeshuka sambamba na dizeli iliyoshuka kwa Sh139 na mafuta ya taa kwa Sh177. Bei ya Dizeli kwa mkoa wa Dar es Salaam ni Sh1,708 na mafuta ya taa Sh1,657.

Januari 7, bei ya petroli ilishuka kwa Sh74 kwa lita, dizeli Sh62 na mafuta ya taa Sh54.

“Bei hii inayoanza kutumika kesho (leo) inatokana na kushuka kwa mafuta hayo katika soko la dunia… Desemba mwaka jana, bei ilichelewa kubadilika katika soko la ndani kwa sababu ya mchakato wa usafirishaji,” alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe na wadau wengine wamekuwa wakisema kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia hakulingani na bei za ndani.

Ngamlagosi alisema bei ya jumla ya petroli imeshuka kwa Sh186.89 kwa lita, dizeli Sh138.97 na mafuta ya taa Sh176.64.

Ngamlagosi alieleza bei ya mafuta masafi ilivyopungua kwenye soko la dunia kuanzia Julai hadi Desemba 2014 na kiasi cha fedha kwenye mabano kuwa ni petroli (Dola 440) kwa tani, dizeli (Dola 304) na mafuta ya taa (Dola 324).

Alisema katika kipindi husika thamani ya shilingi ya Tanzania kulingana na Dola ya Marekani ilishuka kwa asilimia sita: “Bei ya mafuta kwenye soko la ndani ingeweza kupungua zaidi kama thamani ya shilingi isingeendelea kushuka.”

Alisema bei ya mafuta katika soko la dunia ni asilimia 60 wakati gharama za usafirishaji, kodi na bima ni asilimia 40 ambayo haijabadilika.

Alisema kutokana na gharama za usafirishaji kutobadilika, kiwango cha ushukaji wa bei ya mafuta katika soko la ndani hakiwezi kulingana na kile kinachoshuka katika soko la dunia.

Ewura ilisema bei ya jumla ya petroli kwa jiji la Dar es Salaam ni Sh1,666.43, dizeli Sh1,605 na mafuta ya taa Sh1,554.59.

Alisema kutokana na gharama kubwa za usafirishaji, wakazi wa Kyerwa mkoani Kagera ndiyo watakaokuwa wakinunua petroli kwa bei kubwa zaidi ya Sh2005, dizeli Sh1,945 na mafuta ya taa Sh1,894.

Alisema bei mpya ya petroli katika jiji la Mbeya itakuwa Sh1,875, wakati dizeli ni Sh1,814 na mafuta ya taa Sh1,763.

Ngamlagosi alisema Manispaa ya Kigoma bei ya petroli itakuwa Sh1,941, dizeli Sh1,938 na mafuta ya taa Sh1,887.

Aliwakumbusha wamiliki wa vituo vya mafuta kuchapisha bei ya bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana kwa wateja na kuwataka wanunuzi wa mafuta kudai risiti kuthibitisha ununuzi.

Alisema kampuni za kuuza mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta kwa ushindani ili mradi bei hizo ziwe chini ya bei kikomo.

Mkurugenzi huyo alisema mamlaka hiyo iko kwenye mchakato wa kuangalia kama kuna uwezekano wa kupunguza gharama za umeme kutokana na punguzo hilo na mafuta

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana