Featured

    Featured Posts

WAPENZI JINI KABULA NA BUSHOKE WAMWAGANA NA HAKUNA CHA NDOA TENA



Msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.


MSANII wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, Ruta Maximilian Bushoke wamemwagana na hakuna cha ndoa tena.


Akizungumza na Uwazi, Kabula alitoa ya rohoni na kusema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona mwenzake haoneshi msimamo katika mkakati wao wa kuoana hivyo kwa sasa wamebaki kuwa marafiki wa kawaida tu kwa sababu wote ni wasanii.
“Tumeshaachana, mwaka huu nimeuanza kwa kuwa bize na mambo yangu mengine ya kikazi siyo mapenzi tena. Tulikuwa tumepanga vizuri kwamba tutaoana na kuamini hivyo kwa kipindi chote alichokuwa nchini Afrika Kusini.”
“Baada ya mwenzangu kutua Bongo, hakuonesha dalili yoyote ya kutekeleza hilo suala la ndoa. Sikuwa na uwezo wa kusema nimfunge kamba ndiyo nimlazimishe kumpeleka kwetu tuoane, nimeona bora niachane naye kwani nimeshachoka na maisha ya uzinifu nahitaji kuingia katika ndoa,” alisema Kabula.
Bushoke alipotafutwa kwenye simu hakupatikana lakini kwa mujibu wa marafiki zake wa karibu wanasema kuwa amesharudi Afrika Kusini.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana