MAMBO si mambo! Tayari mimba ya muigizaji Aunt Ezekiel imeanza kumtibua baada ya nyota huyo kushindwa kufanya baadhi ya kazi ambazo alikuwa akizifanya mwenyewe.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kutokana na tumbo kuwa kubwa, Aunt kwa sasa hawezi kufunga viatu vyake, kufua, kuosha vyombo na hata akitaka kwenda toileti inabidi apewe kampani na mtu.
“Mh! Jamani Aunt hata kuinama ni mtihani sasa sijui kama ni kujidekeza au nini maana anapokuwa karibu na bebi wake ndiyo usiseme ni full kudeka anasema akiinama anaumia jamani?“Eti sasa hivi shosti wake Wema Sepetu na bebi wake Mose Iyobo ndiyo wamekuwa wakifanya kazi ya ziada kumsaidia kila kazi nyingi anazoshindwa,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kupenyeza habari, paparazi wetu alimsaka Aunt na kufanikiwa kumnasa kwa nyakati tofauti akiwa anasaidiwa kufungwa viatu na Wema pamoja na Iyobo.Alipoulizwa Aunt kama anashindwa kweli kufanya kazi mwenyewe au anadeka, alifunguka:
“Jamani hivi niiname nimkunje mtoto wangu bila sababu za msingi na watu wapo ambao wanaweza kunisaidia kwa nini nijiumize, acheni nisaidiwe,” alisema Aunt.Kwa upande wake, Mose ambaye inaaminika kuwa ndiye mhusika wa mimba hiyo ya Aunt alipozungumza na mwanahabari wetu, alijisifu na kusema anafurahi kuwa baba bora wa Aunt.
Post a Comment