Featured

    Featured Posts

ZAMARADI AWAGUSA MASTAA WA BONGO,SOMA HAPA ALICHOSEMA

JIFUNZE kutokumuona mtu WA AJABU kwasababu lake limeonekana tu WAZI.. jiulize una mangapi unayoyafanya KWA SIRI KUBWA ambayo yanaweza yakashangaza ulimwengu!??? Jibu unalo... mengi!! Ila unajiona msafi sababu tu halijawa dhahiri!! Hivyo usimuone yoyote wa ajabu kwa aliyoyafanya sababu hata wewe unayafanya katika style yako.. ila una uwezo wa KUJIKAUSHA kwenye kundi la watu na kumnyooshea mtu kidole sababu yake YAMEDHIHIRIKA WAZI!!! Jiulize vipi yako yakijulikana.. kwa uyafanyayo unahisi DUNIA itakuangalia vipi!!? Usijione msafi ama mwenye haki ya kusakama mtu kwakuwa tu yako HAYAJADHIHIRIKA!!! Mfanyaji ni mfanyaji tu iwe hadharani ama gizani hivyo usije ukahukumu na kusherehekea ya mtu wakati wewe una MAZITO kuliko ya huyo
yaliyodhihirika.. kuna watu wanaoheshimika SANA kwenye jamii... lakini nyuma ya pazia wanafanya vitu ambavyo hata wao wanajishangaa.. kinachowalinda ni heshima tu na kufanya kwa siri ila mwisho wa siku hakimu wetu ni mmoja tu.. aidha ufanye kwa SIRI ama DHAHIRI!! Hivyo si vizuri kujikausha kwa kumuona mwenzio wa ajabu na wewe kujiweka katika kundi la watakatifu kwakuwa tu lako halijashtukiwa.. penda kutunza siri ya mtu ili MUNGU nae akusitiri.. unapomuaibisha mtu jua hata MUNGU atakuaibisha pia.. ficha aibu za watu ili MUNGU afiche za kwako.. na usipende kufurahia na kushabikia matatizo na AIBU za wengine hali ya kuwa una za kwako nyingi zipo chimbo.. be neutral and judge no one..taratibu tutaweza..!!
By Zamaradi Mtetema
Mastaa wengi wameili-Repost andiko hili mitandaoni akiwemo Kajala. Hata wewe nadhani limekufaa pia.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana