Featured

    Featured Posts

HUYU NDIYE MRITHI WA VAN PERSIE

Klabu ya Manchester United imemuuza straika wake namba moja Robin Van Persie kwenda klabu ya Fernabache. 
Tayari wachambuzi wa soka wameeanza kuyataja majina ya mastraika ambao wanaweza kusajiliwa na Man United kama mbadala wa Van Persie

HARRY KANE
Wachezaji wachache wamekuwa na mafanikio msimu kama Muingereza huyu anayecheza kwenye timu ya Uingereza yenye chini ya miaka 21. Ni Sergio Aguero pekee ndiye aliyefunga mabao zaidi Ligi Kuu kuliko Kane msimu uliopita. Kane amefunga mabao 21. Luis Van Gaal yupo tayari kulipa £ 50,000,000 kwa ajili ya Kane ingawaje Tottenham wamesema kuwa hawapo tayari kumuuza.

MULLER
Muller ameonekana hakuridhika kabisa na jukumu alilopewa kulifanya pale Munich msimu uliopita ingawaje bado anabaki kuwa hazina kubwa kwa timu hiyo. Ripoti zinasema kuwa Van Gaal yupo tayari kulipa jumla £ 120m kwa ajili ya Muller.
BENZEMA
Mpango Rafa Benitez wa kutaka kumchezesha Cristiano Ronaldo mbele kama namba 9 kunaweza kukamfanya Mfaransa kutaka kuondoka klabuni hapo. Ripoti zinadai kuwa LVG yupo tayari kulipia huduma ya Mfaransa huyo.

CAVANNI
Bado Cavanni hajaweza kabisa kumzidi Zlatan Ibrahimovic kama straika chaguo namba moja klabuni PSG. Kuna hisia kuwa Cavanni hafurahii maisha yake kule Ufaransa hivyo yupo tayari kuondoka muda wowote.

LEWANDOWSKI
Man United tayari wameshaini mchezaji mmoja kutoka Bayern (Bastian Schweinsteiger) na ripoti zinasema kuwa inawezekana Man United wakahitaji saini ya mchezaji huyu ingawaje Bayern wameshasema kuwa hawawezi tena kumruhusu mchezaji wao yeyote kujiunga tena na klabu hiyo msimu huu.
BERAINO
Kijana huyu wa West Brom tayari ameshavutia klabu nyingi kubwa barani Ulaya kama Liverpool na Man United. Kama wachezaji wakubwa aliopanga kuwasajili atashindwa, basi LVG anaweza kumsajili kinda huyu.
BENTEKE
Mbelgiji huyu yupo zaidi kwenye rada za Liverpool ingawaje ripoti zinasema kuwa hata Man United wanamvizia kwa karibu sana.

HIGUANI
Murgentina huyu amekuwa akihusishwa na timu za Uingereza kwa muda mrefu sasa. Na baada ya Napoli kushindwa kufuzu UEFA na kumpoteza kocha wao Rafa Benitez basi kuna uwezekano mkubwa wa yeye kujiunga na timu za Uingereza na tayari Man United wameshaonesha nia ya kumtaka.
LACAZETTE
ni Messi na Ronaldo ndio wamemzidi magoli mchezaji huyu kwa msimu uliopita. Hali imevifanya vilabu vikubwa kuanza kunyemelea saini ya mchezaji huyu anyekipiga katika klabu ya Lyon ya Ufaransa.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana