Featured

    Featured Posts

TAARIFA YA KUSIKITISHA YA KIFO CHA MWANAFUNZI UDSM, AKANYAGWA NA MAGARI MATATU


Ndugu zangu wana UDSM nasikitika kuwapa taarifa kuwa  jana usiku wa saa tano na dakika 20 nilishuhudia mwana UDSM mwenzangu akigongwa na gari ndogo nyeusi maeneo ya njiapanda ya chuo Ubungo  gari iliyombuluza mita kadhaa kisha kusimama kurudi nyuma na kutokomea kusipojulikana baada ya makelele tuliyopiga, mbaya zaida gari la pili lililokuwa kasi nalo likamkanyaga kisha la tatu nalo likamkanyaga ndipo tulipoamua kusimama katikati ya barabara ilikuzuia maumivu zaidi kwa mtu ambaye MPAKA WAKATI HUO SIKUJUA NI NANI
Nilikuwa mimi na naibu wangu Joel ntile, tukaamua kukata majani ili kuzuia magar yaliyokuwa yanakuja kwa kasi kutokana na kutokuwepo kwa foleni usiku ule katika barabara ya  kutoka mwenge kwenda ubungo mataa.
Tukishirikiana na wananchi wengine, tulianza kutafuta gari la kumbeba huyu mtanzania mwenzetu ambaye mpaka muda huo hatukujua ni nani, lakini kila tuliyekuwa tukimwomba msaada hakutusaidia na nilipojaribu kupiga simu polisi haikupokelewa mpaka tukapata akili ya kumkagua aliyegongwa kujua anandugu na jinsi gani watafika tushirikiane kumpa msaada, MPAKA MUDA HUO BADO SIKUJUA KUWA NINAYEMSAIDIA NI MWANAFUNZI MWENZANGU.
Tulipo ipata simu yake tayalri ilikuwa imezimika baada ya kupondwa na magari matatu, tukatoa line na kuiweka kwenye simu nyingine kila namba tuliyojaribu haikupokelewa, wakati huo tuliazimia kufunga barabara ili police wasikie japo kilio chetu na kila tukipiga simu yao iliendelea kupiga wimbo uleule.
Mpaka tulifanikiwa kupata namba iliyoseviwa shem, tulipopiga alipokea na nilistushwa na kauli kuwa yupo mabibo na mwenyesimu ni mwanafunzi mwenzake wa UDSM mwaka wa nne COET, NILIVURUGIKA AKILI
Mpaka muda huo ilikuwa tayari saa nzima imepita bila msaada ndipo nikapiga simu haraka kwa raisi wa DARUSO mh Ahadi Kitaponda, naye akatuma gari la wasaidizi wapolisi na dakika chache akaja na ambulance lakini mpaka muda huo tayali tulikuwa tumechelewa sana na mwana zuoni huyu alikuwa amesha achana na ulimwengu huu wa shida na mateso,
Polisi walikuja baadae sana kama saa saba kasoro wakiwa na bunduki na mabomu mithili wanakwenda kupambana na wahalifu, lakini kuja kwao hakukusaidia kitu.  Ndipo tulianza kuandaa utaratibu wa kwenda kumpumzisha kwa muda  ndugu yetu muhimbili kwa kuanza na dispensari ya chuo na baadae mida ya saa tisa na nusu tukaingia muhimbili tukiwa na viongozi wa DARUSO pamoja na jamaa na watu wakaribu wa marehem na mpaka saa kumi na dakika arobaini tulikuwa tunarudi chuo na hatimaye mabibo." Alieleza shuhuda huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana