Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja akikata mauno.
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni maeneo ya Twende Polepole, Mkoa wa Pwani kwenye sherehe ya kumkaribisha mtoto wa mwigizaji Aunt Ezekiel (Baby Shower) iliyohudhuriwa na watu wengi akiwemo Kajala.
Awali, mwanahabari wetu aliyekuwa akikusanya matukio eneo hilo alimshuhudia Kajala akipata ‘kilaji’ kisha akaitwa na mshereheshaji Maimartha Jesse na kupewa nafasi ya kucheza muziki ndipo alipoanza kuionesha tatuu yake iliyopo bajani kabla ya kuanza kukata mauno.
Watu waliokuwepo ukumbini humo walipigwa na mshangao kwani hakuna aliyeamini staa kama huyo alikuwa mahiri wa kuzungusha nyonga.“Yaani ni balaa, sijui ni kuzidisha kilaji au ni vipi, mtoto wa kike kajitoa ufahamu kwelikweli, leo ndiyo amefunika watu wote hapa,” alisema mmoja wa waalikwa.
“Aunt Ezekiel kwa kushirikiana na marafiki zake, waliamua kufanya sherehe kwa lengo la kufurahi pamoja na kumpa mwigizaji huyo zawadi mbalimbali za mtoto wake mtarajiwa.
Mbali na Kajala, sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kadhaa akiwemo Husna Idd ‘Sajenti’ (mwigizaji), Nice Chande (muigizaji), Zamaradi Mketema (mtangazaji) na wengineo ambao nao walicheza muziki, kula na kunywa.
Post a Comment