MCHAPO KAMILI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo ‘anko’ huyo ambaye ni dereva wa magari ya benki maarufu jijini Dar, alidaiwa kumsumbua binti huyo wa sekondari kwa muda mrefu.
Ilisemekana kwamba, kwa mujibu wa binti huyo, anko wake alikuwa akimnunulia soda baridi na kumuahidi kuendelea kumfanyia hivyo endapo atakubali ombi lake.
...Anko akiwa amewekwa chini ya ulinzi.
Ilidaiwa kwamba, baada ya kuona usumbufu umezidi, binti huyo aliamua kukisanua kwa mzazi wake ndipo mtego bab’kubwa’ ukawekwa. MAKUTANO GESTI
Baada ya mzazi kumpa mbinu zote za kuhakikisha hajirahisishi kwa mjomba wake, alitakiwa kumseti ili aumbuke ndipo binti akakubaliana na mjomba huyo wakutane gesti (jina kapuni) iliyopo maeneo hayo ya Mzambarauni.
KIBANO
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mjomba mtu akiwa anajiandaa ‘kumtoa kafara’ mtoto wa dada yake ndipo dada mtu na shemeji yake wakaibukia gesti chumba namba 02 na kuzua timbwili la kukata na mundu kwa kumtia mtuhumiwa mikononi kwa msaada wa polisi.
Baada ya kutiwa mikononi na baba wa mtoto wa kike, aliamua kumpeleka hadi kwa askari mmoja anayelinda benki na kumpaki gari kwa lengo la kumpeleka mtuhumiwa kwenye kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya Mzambarauni.
Hadi ‘shushushu’ wetu anaondoka kituoni hapo, jamaa huyo alikuwa akihojiwa huku akiomba suala hilo wakalimalize nyumbani.
Post a Comment