Featured

    Featured Posts

MRISHO NGASSA ASAJILIWA NA KLABU HII KUBWA NCHINI AFRIKA KUSINI



KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania
Mrisho Khalfan Ngassa amesaini Mkataba wa
miaka minne kujiunga na klabu ya Free State
Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini leo.
Ngassa, mume wa Radhia na baba wa Farida (8)
na Faria (6) aliwasili jana jioni mjini hapa na leo
asubuhi baada ya kukamilisha mazungumzo,
akasaini Mkataba huo mnono.
“Nimefurahi kusaini timu hii, ambayo kaka yangu
Nteze John amewahi kuchezea pamoja na
wachezaji wengine wakubwa kama Tshabalala n
Mweene,”alisema Ngassa.
“Sasa najiandaa kwa maisha mapya baada ya
kucheza Tanzania kwa muda mrefu, hii ni
changamoto mpya kwangu, mpira wa Afrika
Kusini upo juu sana ukilinganisha na pale kwetu
(Tanzania). Nataka kutumia fursa hii kuitangaza
soka ya Tanzania, ili klabu zisijifikirie tena kusaji
wachezaji wa Tanzania,”amesema Ngassa.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu hiyo
maarufu kama Ea Lla Koto, Mmalawi Kinnah Phir
amesema kwamba amekuwa akimpenda Ngassa
kwa muda mrefu na kukutana naye FS ni kutimia
kwa ndoto zake za kufanya kazi na kijana huyo
siku moja.
Katika Mkataba huo ambao Ngassa, mtoto wa
kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa
atakuwa analipwa karibu mara tatu ya mshahar
aliokuwa anapata Yanga SC, atapatiwa nyumba
ya kuishi na familia yake, gari na huduma
nyingine muhimu, ikiwemo bima.
Ngassa anakuwa Mtanzania wa pili kuichezea
Free State, baada ya Nteze John Lungu ‘mwana
Mwanza’ pia aliyeichezea timu hiyo enzi hizo
inaitwa Qwa Qwa Stars mwaka 1997 hadi 1999.
Ngassa anatua Free States akitokea Yanga SC,
ambayo ameichezea jumla ya mechi 186 katika
awamu mbili, na kuifungia jumla ya mabao 86.
Ngassa aliyetimiza miaka 26, Aprili 12 mwaka
huu, alijiunga na Yanga SC kwa mara ya kwanza
mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar iliyomuibua
mwaka 2005 kutoka timu ya vijana ya Toto
Africans ya Mwanza.
Mwaka 2010 alihamia Azam FC kwa dau la reko
wakati huo, dola za Kimarekani 40,000 (Sh.
Milioni 80).
Kabla ya hapo, akiwa Yanga SC, Aprili mwaka
2009, Ngassa alikwenda kufanya majaribio klabu
ya Ligi Kuu England, West Ham United wakati hu
chini ya kocha Mtaliano Gianfranco Zola.
Hata hivyo, pamoja na mshambuliaji wa zamani
wa Chelsea, Zola kuvutiwa na uwezo wa mcheza
huyo kisoka, akasema Ngassa anahitaji kurejea
Afrika kuongeza lishe.
Julai mwaka 2011, Ngassa alikwenda kufanya
majaribio Seattle Sounders FC ya Ligi Kuu ya
Marekani na akatumiwa katika mchezo wa
kujiandaa na msimu dhidi ya Manchester United
ya England.
Hata hivyo, Azam FC haikuwa tayari kumuuza
mchezaji huyo. Ngassa alicheza Azam FC hadi
mwaka 2012 alipohamia Simba SC kwa mkopo n
mwaka 2013 akarejea timu yake kipenzi, Yanga
SC ambayo, ameiaga baada ya msimu akiiachia
ubingwa wa Ligi Kuu.
Mfungaji huyo bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika
msimu uliopita, pia amewahi kuwa Mchezaji Bor
wa Tanzania mara mbili mwaka 2010.
Mwaka 2005 akiwa Kagera Sugar alishinda
Kombe la Tusker wakiifunga Simba SC katika
fainali na alipohamia Yanga SC alishinda mataji
ya Ligi Kuu katika misimu ya 2008, 2009 na
2015.
Ameshinda pia mataji ya Tusker mwaka 2007 na
2009 akiwa na Yanga SC, wakati akiwa na Azam
FC aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya pili
katika Ligi Kuu na Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame mwaka 2012.
Amekuwa Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodaco
Tanzania Bara msimu wa 2010–2011 akiwa na
Azam FC na mfungaji bora wa Kombe la
Challenge mwaka 2009.
Huyo ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu mwezi
Apirli mwaka huu, ambaye ana nafasi kubwa ya
kuwa pia Mchezaji Bora wa jumla wa Ligin Kuu
msimu huu.
Amekuwa mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars tangu mwaka 2007 na had
sasa amiechezea timu hiyo mechi 82 na kuifungi
mabao 22.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana