Featured

    Featured Posts

AJIRA ZA WALIMU MWAKA 2015



Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa, kwa Maelekezo zaidi tafadhali soma tangazo lililo mwishoni.
FUNGUA MAJINI YOTE KWA KUBOFYA LINK ZA HAPA CHINI....
Ajira za Walimu wa Masomo ya Sanaa na Biashara Ngazi ya Shahada na Stashahada.

AJIRA MPYA YA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA NA WALIMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2014/15

A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;
ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari
iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo
ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari


B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14
wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na
hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi
wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;
iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari,
cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari
(ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
 

Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana