Wakati Askofu wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima, Josephat Gwajima akijisalimisha kwa Jeshi la Polisi, Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka aripoti ofisini kwake
keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi
mwenzake wa dini.
Makonda amemwandikia barua
Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya
maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.
Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake
inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu
wengine. “Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka
sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema.
Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini.”Anadaiwa kuzimia jana alipokuwa akihojiwa na Polisi kwa tuhuma za kumkashfu Kardinali Pengo.
Post a Comment