Dar es Salaam. Matukio ya wasafiri kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiwa na nyara za Serikali na dawa za kulevya, yanazidi kuchukua sura mpya baada ya raia mmoja wa Ubelgiji kukamatwa akiwa na fuvu la binadamu.
Raia huyo, Balcjan Christine Weejktgns (49), alikamatwa Jumatatu saa 2.30 usiku wakati akiwa katika taratibu za kuingia uwanjani hapo tayari kwa safari ya kuelekea Ubelgiji kupitia Zurich, Uswisi.
Kwa maelezo yake alidai kuwa fuvu hilo analimiliki muda mrefu tangu alipoingia nchini mwaka 2000 akitokea Ubelgiji akidai kuwa yeye ni mtafiti.
Post a Comment