MFANYAKAZI wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella amevamiwa na majambazi wenye silaha na kupigawa risasi, kujeruhiwa na kisha kuporwa fedha zake mchana huu maeneo ya Tabata-Relini jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Pella anadaiwa kuporwa kiasi cha Sh. Mil 2 alizokuwa nazo akiwa ametoka kuzichukua kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) Tawi la NMB liliyopo jirani na Azam TV, Barabara ya Mandela.
Mtandao huu ulimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki kuelezea zaidi tukio hilo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Post a Comment