Featured

    Featured Posts

BREAKING NEWS: RAIS DK JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27, SHABANI KISU, PAUL MAKONDA,F REDRICK MWAKALEBELA WAPATA NEEMA. 18 Feb 2015 / 0 comments MTOTO ALBINO ALIYEPORWA KUTOKA MIKONONI MWA MAMA YAKE AUAWAWA, MAITI YAKUTWA HAINA MIGUU NA MIKONO 18 Feb 2015 / 0 comments WANANCHI WAHOJI UWEZO WA INTELIJENSIA YA POLISI BAADA YA MAJAMBAZI KUTAMBA NA KASI YA UPORAJI TANZANIA. 18 Feb 2015 / 0 comments MTOTO ALBINO AIBWA BAADA YA MAMA YAKE KUCHARANGWA MAPANGA CHATO MKOANI GEITA. 17 Feb 2015 / 0 comments NI TAHARUKI JUU YA MASWALI 10 YA UVAMIZI ENEO LA AMBONI YALIYOACHA UTATA TANGA. 17 Feb 2015 / 0 comments DAWA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA TFDA ZAZAGAA MITAANI NA KUUZWA MWANZA. 17 Feb 2015 / 0 comments KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA HARDNEWS JUMANNE YA FEBRUARI 17 / 2015, IKIWA NA VICHWA VIKUU VYA HABARI. 17 Feb 2015 / 0 comments KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA UDAKU JUMANNE YA FEBRUARI 17 / 2015, IKIWA NA VICHWA VIKUU VYA HABARI. 17 Feb 2015 / 0 comments TASWIRA MSIBA WA BABA 'YAKE DULLY SYKES' KAWE BEACH JIJINI DAR ES SALAAM LEO. 16 Feb 2015 / 0 comments TANZANIA SASA HALI SI SHWARI, TUKIO LA AMBONI TANGA LAWASTUA WANANCHI. 16 Feb 2015 / 0 comments RAIS DK JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27, SHABANI KISU, PAUL MAKONDA,F REDRICK MWAKALEBELA WAPATA NEEMA. MTOTO ALBINO ALIYEPORWA KUTOKA MIKONONI MWA MAMA YAKE AUAWAWA, MAITI YAKUTWA HAINA MIGUU NA MIKONO WANANCHI WAHOJI UWEZO WA INTELIJENSIA YA POLISI BAADA YA MAJAMBAZI KUTAMBA NA KASI YA UPORAJI TANZANIA. MTOTO ALBINO AIBWA BAADA YA MAMA YAKE KUCHARANGWA MAPANGA CHATO MKOANI GEITA. NI TAHARUKI JUU YA MASWALI 10 YA UVAMIZI ENEO LA AMBONI YALIYOACHA UTATA TANGA. DAWA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA TFDA ZAZAGAA MITAANI NA KUUZWA MWANZA. KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA HARDNEWS JUMANNE YA FEBRUARI 17 / 2015, IKIWA NA VICHWA VIKUU VYA HABARI. KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA UDAKU JUMANNE YA FEBRUARI 17 / 2015, IKIWA NA VICHWA VIKUU VYA HABARI. TASWIRA MSIBA WA BABA 'YAKE DULLY SYKES' KAWE BEACH JIJINI DAR ES SALAAM LEO. TANZANIA SASA HALI SI SHWARI, TUKIO LA AMBONI TANGA LAWASTUA WANANCHI. RAIS DK JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27, SHABANI KISU, PAUL MAKONDA,F REDRICK MWAKALEBELA WAPATA NEEMA.

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/09/Rais-Jakaya-Kikwete.jpg
RAIS DK KIKWETE.

Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani.


RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani. 


http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/Mizengo-Pinda.jpg
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.


Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.


Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.


Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).


Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).


Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).


Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, FEBRUARI 18, 2015.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana