Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Musa hivi karibuni alichezea kichapo cha nguvu kisha kung’olewa meno kwa koleo baada ya kunaswa akitaka kuiba nyumbani kwa mtu.
Kijana Mussa akiwa hoi baada ya kung'olewa meno.
Tukio hilo lilitokea katika mji mdogo wa Tunduma uliopo wilayani Momba mkoani hapa ambapo kijana huyo alinaswa akiingia kwenye nyumba iliyopo Mtaa wa Tazara, Kata ya Kaloleni ya mtu aliyefahamika kwa jina la Mahinya.
Chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza: “Yule jamaa alionekana mara ya kwanza akiingia kwenye nyumba ya Mahinya, aliposhtukiwa akakimbia.“Kama vile haitoshi mida ya saa 10.30 jioni akarudi tena akitaka kuiba na ndipo watu walipomkamata na kumpa kipigo.
Akiwa mikononi mwa polisi.
“Akaminywa sehemu za siri kisha akang’olewa meno kwa koleo na baadaye akapelekwa Kituo Kidogo cha Polisi Tunduma kwa hatua za kisheria lakini akiwa nyang’anyang’a.”
Post a Comment