Featured

    Featured Posts

BREAKING NEWS: WATU NANE AKIWEMO MAMA MJAMZITO WAMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUNYWA MAZIWA YENYE SUMU SINGIDA


Watu nane wa familia tatu akiwemo mama mjamzito wa kijiji cha nkuhi wilayani ikungi,wamenusurika kufa baada ya kunywa maziwa yanayo sadikiwa kuwa na sumu.
Wakieleza kwa shida  akiwemo aliye wauzia maziwa  hayo huku wakiwa wamelazwa katika hospitali teule ya masister wa malikia wa ulimwengu iliyopo katika kijiji cha puma ,wamesema baada ya kunywa maziwa hayo walianza kuumwa na tumbo huku wakiharisha na kutapika kwa mfululizo
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya masister wa malikia wa ulimwengu Daktari Corbinian Nyenyembe,amesema wamepokea wagonjwa wanao sadikiwa kunya sumu  wa familia tatu akiwemo mama mmoja ambaye ni mjamzito,watu wakubwa watatu na watoto  wanne ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi mkiwa wilayani ikungi,baadhi yao wakiwa na halimbaya na wanaendelea na matibabu.
Bwana Jeremia Saudi ni baba wa watoto watatu walio kunywa maziwa  na wamelazwa katika hospitali hiyo ,amesema wamebaini kuwa maziwa hayo yanaweza kuwa na sumu baada ya kaka yake kuyaonja na kukuta siyo kama maziwa mengine.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana