Jolly Tumuhirwe akiwa mahakamani leo.
Jolly Tumuhirwe alipokuwa akimtesa mtoto Arnella.
HAUSIGELI aliyenaswa kwenye video akimtesa mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe ameiambia mahakama kuwa anajutilia kile alichokifanya na anaomba msamaha.Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.
Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Bi.Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Jumatano ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.
Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mia nne au adhabu zote mbili.
Post a Comment