ULEVI noma! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusu kilichomtokea mtoto wa kigogo mmoja aishie Masaki ambaye alijikuta akifanyiwa kitu mbaya ndani ya maji kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Coco jijini Dar, Jumamosi iliyopita.
Binti akijiachia na njemba huyo baada ya kupiga urabu wa kutosha.Kabla ya tukio hilo, inadaiwa kuwa dada huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alikesha katika klabu moja iliyopo ufukweni hapo, akipiga ulabu yeye pamoja na kampani yake.Ilipofika asubuhi, inadaiwa kuwa, ili kupunguza ulevi aliokuwa nao kichwani, aliamua kwenda kuogelea, ili akae sawa.
Chanzo kilichoshuhudia tukio hilo kilishadadia maneno kwa mpigapicha wetu kwa kusema kuwa, wakati mrembo huyo anaenda kuogelea ndipo alipoangukia kwenye mikono ya njemba mmoja aliyekuwa akifanya mazoezi pembeni mwa ufukwe huo ambapo pia alikutana na wachezaji wa Azam FC waliokuwa wakifanya mazoezi mambo yakaharibika.
...Akionyesha kufurahia hali hiyo.“Wakati anawafuata wale wachezaji, redio za watu wa bajaj zilikuwa zimefungulia muziki kwa sauti, akawa anacheza, jamaa walipoona vile wakaongeza sauti na kumwekea wimbo wa Davido wa Aye, dah, ndio akachizika kabisa, jinsi alivyokuwa akikata mauno na nguo alizovaa, aliwachanganya kabisa wachezaji wa Azam ambao walikuwa wakimtumbulia macho kwa udenda,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuwapagawisha wachezaji hao, binti huyo alipomfuata njemba mmoja aliyekuwa kando na kumuomba amfundishe kuogelea, jamaa akachukua tairi la gari na kumwingiza baharini ambako alianza makeke ya kumfundisha huku wakizamia kuonesha kuna kamchezo kachafu kanaendelea.
Baadaye akiwa kama aliyeshtuka, alikurupuka majini humo na kutoka nje akikimbia, akimuacha njemba aliyekuwa naye baharini akimtumbulia macho ya kutoamini kilichotokea.
Post a Comment