Featured

    Featured Posts

PICHA ZINATISHA: MOMBASA HALI NI TETE,MSAKO WA POLISI MISIKITINI VIJANA WANNE


KIJANA alipigwa risasi na kuuawa na wenzake
zaidi ya 250 kukamatwa kwenye operesheni
kali ya kusaka magaidi mjini Mombasa jana.
BAADHI ya vijana waliokamatwa ndani ya
misikiti ya Musa na Sakina, eneo la Majengo,
Mombasa, wakati wa msako wa polisi usiku
wa kuamkia jana ambapo kijana aliuawa na
washukiwa zaidi ya 251 kukamatwa.Silaha
mbalimbali zikiwemo gruneti, bastola, visu na
mapanga zilipatikana ndani ya misikiti hiyo.
Akihutubia wanahabari katika kituo cha polisi
cha Urban, mjini Mombasa, afisa mkuu wa
polisi
(OCPD) Mahmoud Salim, alisema kijana
aliyeuawa alijaribu kushamulia maafisa wa
usalama kwa gruneti walipokuwa wakiingia
msikitini. “Walimpiga risasi kabla ya hajatupa
gruneti hiyo na kumwua papo hapo,” akasema
Bw Salim na kuapa kuwa operesheni hiyo
itaendelea hadi wahalifu wote wanaswe.
Vijana 16 walikamatwa ndani ya msikiti wa
Masjid Musa na wengine wanane
wakapatikana kwenye msikiti wa Sakina.
Wakati huohuo, viongozi wa eneo la Mombasa
wametaka vijana waliotiwa mbaroni waachiliwa
mara moja kama hawatapatikana na hatia.
Wakiongozwa na gavana Hassan Joho,
viongozi hao walifika katika makao makuu ya
polisi ya kaunti hiyo ambako walishauriana na
maafisa wakuu wa polisi kwa karibu saa mbili.
Walishutumu maafisa wa polisi kwa kuvamia
msikiti wakisema ni mahali patakatifu pa
ibada.
Wengine walikuwa Seneta Hassan Omar,
Mwakilishi wa Wanawake Mishi Juma Mboko
na wabunge Abdulswamad Nassir (Mvita),
Rashid Bedzimba (Kisauni) na Badi Twalib
(Jomvu).
- Taifa Leo
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana