Featured

    Featured Posts

MDAHALO KUHUSU KATIBA MPYA KUNDI LA VIJANA WANAODHANIWA KUWA CCM WAANZISHA VURUGU HADI NGUMI ZAPIGWA WAKATI WA MDAHALO

warioba
Jaji Warioba.
VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea hivi punde katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
Vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.
 Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV umesimamishwa kwa muda. 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana