Baada ya wale polisi traffic waliojipiga picha wakiwa katika pozi ya mahaba wakati wakiwa kazini kusambaa sana mtandaoni , picha nyingi za vituko za walinda usalama wetu zimekuwa zikisambazwa mtandaoni kuonyesha namna gani polisi wetu wanavyoacha kazi zao na kufanya vituko. Tazama picha hii ya polisi huyu akiwa ameshika chupa ya pombe wakati bado akiwa kazini .
Siku zote tumekuwa tukilalamika kuhusu ajali za barabarani, lakini kumbe polisi wenyewe ni chanzo cha matatizo hayo, Mfano , huyu polisi baada ya kulewa ataweza kweli kuchunguza gari na kujua kama lina matatizo au la ? ataweza kumkamata dereva ambaye nae anaendesha gari huku akiwa amelewa?
Ni vema serikali na mamlaka zingine zinazohusika kuhakikisha zinaajiri polisi ambao wataafuta viapo vya kazi zao, na wale wanaokwenda kinyume na sheria za kazi zao wachukuliwe hatua kali mara moja.
Post a Comment