Mwanariadha
mlemavu, Oscar Pistorius aliyehukumiwa miaka mitano jela,leo October
21,2014, tayari ameingia kwenye gereza kongwe la Kgosi Mampuru II
Prison.
Gereza hilo liko jijini Pretoria na linajulikana kutokana na kuwa na sifa ya kuhifadhi vijana watukutu.
Mwanariadha huyo amehukumiwa kutokana na kumuua mpenzi wake bila kukusudia.
TAZAMA MAZINGIRA YALIVYO...
|
|
Mwanariadha
wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 leo October
21,2014, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva
Steenkamp.
|
|
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wakeReeva Steenkamp enzi za uhai wake.
Hii
ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya kumuua
mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka uliopita bila ya kukusudia.
Jaji
aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya
mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni
changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote
kwenye kesi hiyo.
|
|
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa.
Upande
wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10
gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande
wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius
wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe
usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
|
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment