MAMIA ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakiongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wamejitokeza kumzika marehemu Method Clecence Mengi aliyeuawa kwa kuchomwa visu na watu wasiofahamika nchini Marekani.
Mama akimuaga marehemu mwanaye, Method Clecence Mengi.
Mengi alikumbwa na ukatili huo wa kuchomwa visu vitatu, tumboni viwili na kwenye paji la uso Septemba 17, mwaka huu nje ya nyumba yake, Texas nchini humo na watu hao bila kujulikana kisa na waliingia mitini baada ya tukio hilo la kikatili.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude akiuombea mwili wa marehemu Method Clecence Mengi.
Mara baada ya tukio hilo, mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi kwenda hospitali kwa uchunguzi mpaka Oktoba 1, mwaka huu ulipotolewa na kuletwa nchini kwa mazishi.Mwili wa Mengi aliyeishi nchini Marekani tangu mwaka 2000, uliwasili nyumbani kwa wazazi wake, alfajiri ya Oktoba 2, mwaka huu na baadaye saa tisa alasiri kupelekwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Patrick kwa ibada ya mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Waombolezaji wakiupokea mwili wa marehemu Method Clecence Mengi kwa ajili ya mazishi
Marehemu alizikwa saa kumi kwenye Makaburi ya Kolla huku akiacha maswali ya namna alivyouawa na mkewe ambaye ni Mmarekani kutoonekana kwenye mazishi wala kuja Bongo.Akizungumza baada ya mazishi hayo, mdogo wa marehemu Ribbon Mkali ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilakala alisema:
Marehemu Method Clecence Mengi (kushoto) enzi za uhai wake
”Ni kweli shemeji yangu, mke wa marehemu hajafika nchini bado yuko Marekani na watoto wake wawili, zaidi ngoja tumalize msiba, tutaongea mengi.”
Post a Comment